App ya kidijitali kwa walimu kusimamia , wanafunzi, na matokeo kwa urahisi
Darasa Langu — description
Darasa Langu Application
Darasa Langu ni programu ya kisasa iliyoundwa mahsusi kwa walimu wa shule za msingi, sekondari, na kidato cha juu. Simamia shughuli zako zote za kufundisha mahali pamoja — bila msongo wa karatasi.
✅ Usimamizi wa Madarasa Unda na simamia madarasa yako kwa urahisi. Ongeza wanafunzi, panga masomo, na fuatilia maendeleo ya kila darasa kwa ufanisi zaidi.
📋 Mahudhurio ya Wanafunzi Rekodi mahudhurio ya kila siku kwa haraka na kwa urahisi. Tambua wanafunzi waliopo, waliochelewa, wenye udhuru au wasiokuwepo — yote kwa muda mchache tu.
📊 Matokeo na Alama Weka na simamia alama za wanafunzi kwa kila somo. Mfumo wa daraja huhesabu na kutoa matokeo automatic kulingana na vigezo ulivyoweka mwenyewe.
📚 Maazimio ya Mitihani Pata na pakua maazimio ya mitihani ya miaka iliyopita yaliyoandaliwa kwa mpangilio wa darasa, somo, na mwaka — kwa urahisi wa kutafuta na kutumia.
📰 Elimu News Kaa karibu na habari mpya za elimu. Soma taarifa, mabadiliko, na matangazo muhimu ya elimu moja kwa moja ndani ya programu.
🔒 Salama na ya Faragha
☁️ Usawazishaji wa Data Data yako husawazishwa moja kwa moja na seva. Hata ukibadilisha simu, taarifa zako zote zitabaki salama na kupatikana kwa urahisi.
Darasa Langu — Teknolojia inayompa mwalimu nguvu zaidi darasani.